Sunday, September 2, 2012

WAISLAMU WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA HIJJA

Taasisi ya maendeleo ya waislamu Tanzania(Islamic Development Centre IDC) inawatangazia waislamu wote kwa ujuma kushiriki katika  Ibada ya Hijja mwaka huu 2012 ambapo Katibu mkuu wa IDC sheik Salim Juma Salim amesema kuwa Gharama  ya kwenda Hijja kwa mwaka huu ni dola 3800 za kimarekani tu zitakazotumika katika safari ya ndege, chakula pamoja na malazi.

Katibu mkuu wa IDC Sheik Salim Juma Salim akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni mratibu wa IDC BW, Majaliwa Suleiman.

Mkurugenzi wa IDC akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambapo aliwasisitizia waislamu kushiriki katika ibada hiyo ili kuyabadilisha maisha yao yaendane na maadili ya kimungu.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria wakipiga kazi