Sunday, September 2, 2012

BUNGE LA AFRICA MASHARIKI KUANZA KESHO NAIROBI NCHINI KENYA

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Africa Mashariki  wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo hii jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bunge la Africa Mashariki Mh, Adam Kimbisa, akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam ambapo amewataarifu wananchi kuwa kesho watakwenda nchini Kenya kwa ajili ya kikao cha Bunge kitakachoanza Nairobi  Kesho.
Jumla ya Wabunge wa Bunge la Africa Mashariki kutyoka Nchini Tanzania wapo tisa katika vyama mbalimbali ikiwemo  CCM, Chama cha wananchi CUF, pamoja na NCCR Mageuzi.

Watanzania wajasiriamali wametakiwa kuchangamkia soko la Afrika Mashariki ili kila mtanzania aweze kufaidika katika soko la Afrika Mashariki.

Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki Mh, Shairose  Bayi akizungumza katika mkutano huo.

Huyu naye ni Bi, Anjela Kiziga katika mkutano huo.