Saturday, September 15, 2012

TPDC AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI

Waziri wa Nishati na Madini Bw, Sospiter Muhongo, akiwa kwenye mkutano wa kuzindua Bodi ya  Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) iliyozinduliwa leo katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam ambapo waziri aliishauri bodi hiyo kuakikisha kuwa faida kubwa  itakayopatikana katika Petroli iingie katika soko la Tanzania. Pia ameitaka Bodi hiyo  kuhakikisha kuwa wawekezaji watakao wekeza wanatoka ndani ya Tanzania na sio wawekezaji kutoka Nje ya Tanzania.