Monday, September 17, 2012

TFDA YABAINI WATOTO WA IRINGA KUATHIRIKA NA SUMU KUVU;, WAMWELEZA WAZIRI WA AFYA ALIPOTEMBELEA TFDA LEO

Waziri wa Afya nchini Tanzania Dk Hussein Mwinyi kushoto akiongozana na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Bw Hiiti Sillo kulia wakati waziri wa Afya alipotembelea TFDA leo jijini Dar es Salaam ambapo mkurugenzi.wa TFDA ameiombba wizara ya Afya kuendelea kuwaunga mkono ili TFDA iweze kutimiza jukumu la kulinda afya ya jamii.

Kaimu mkurugenzi wa Chakula bora (food safety) Bw, Martin Rimanya akimuelekeza waziri aina ya vyakula walivyo vifanyia uchunguzi ambapo amesema kuwa  kuna jumla ya vyakula 3018 ambavyo vimesajiliwa baada ya kufanyiwa uchunguzi na pia amesema kuwa kuna majengo 5025 ambayo yapo tayari kukagua vyakula nchini na kuongeza kuwa watu na makampuni , yanayotakiwa kuingiza chakula nchini ni watu 1431 tu. Aidha Bw, Rimanya ameongeza kuwa  wamefanya uchunguzi katika mikoa kumi ili waweze kubaini ni watu kiasi gani walio athirika na sumu inayopatikana katika  vyakula zinazotokana na ukungu maarufu kama sumu kuvu na kubaini kuwa Mkoa wa Iringa umeathiriwa zaidi na sumu hiyo.

Mkurugenzi wa huduma za maabara TFDA Bi, Charys Ugullum akimuelekeza waziri wa Afya Dk Hussein Mwinyi,  namna Maabara inavyofanya kazi yake ya kupima madawa na chakula.

Kaimu Mkurugenzi wa Dawa na Vipodozi TFDA Bw, Henry Irunde akimwonyesha Waziri document inayoelezea  majaribio ya dawa mbalimbali zikiwemo dawa za kienyeji.


Wafanya kazi wa TFDA