![]() |
Joseph Mapunda (kushoto) na Mama yake Mazai, ambaye pia ni mkewe, Condrada Ngonyani (kulia) |
HabariLeo -- KIJANA kwa miaka 10 sasa, aliridhia kuacha mkewe na watoto ili kufaidi penzi la mama yake mwenye umri wa miaka 70.
Joseph Mapunda (40), ameliambia gazeti la Habari Leo katika kijiji cha Namabengo, wilayani Namtumbo hivi karibuni, kuwa, kabla ya 'kuoza kimapenzi’ kwa mama yake, Condrada Ngonyani, alikuwa mume wa mtu na alibahatika kuzaa na mkewe huyo watoto wawili.
Hata hivyo, alifichua kuwa, kutokana na penzi lake kuelemea kwa mama mzazi, mkewe alibaini lakini haikusaidia, kwani alishaamua liwalo na liwe. Ndipo kwa hasira, mkewe aliondoka na watoto na mpaka sasa hajui iliko familia yake hiyo. Mapunda alisema ingawa jamii imekuwa ikiwasuta na kuwashangaa kwa kuingilia penzi lao, wao hawaoni kama kuna jambo la ajabu katika hilo. Aliongeza, kuwa amekuwa akifurahia maisha katika kipindi chote alichoishi na mama yake kama mke na kitu pekee ambacho hawajafanikiwa katika uhusiano wao ni mtoto.
Anasema walianza kuishi kama mume na mke baada ya kukubaliana na mzazi wake huyo, kutokana na kuvutiwa naye, akalazimika kumshawishi na ndipo Mama aliporidhia na kuanzisha penzi linalotimiza miaka 10 sasa.
Mama huyo naye alikiri kuridhia kuangukia katika penzi la mwanawe, huku akisisitiza kumpenda kuliko hata alivyokuwa anampenda mumewe-Baba Joseph, ambaye kwa sasa ni marehemu. Aliongeza, kuwa anashangaa wanaoshangazwa na penzi lao, akisema licha ya kuwa si la kawaida kwa mila za kiafrika, lakini hakuna tatizo kwani muda wote walioishi hakuna jambo baya lililowatokea, hivyo kujikuta wakiendelea na maisha ya kawaida kama ya watu wengine ambao wako kwenye ndoa, "Kwani kuna tatizo katika jambo hili? Mimi naona ni sawa na watu wengine tu walioko katika uhusiano wa kindoa, kama ingekuwa niko na mwanamke mwezangu sawa, lakini huyu mtoto wangu ni mwanamume kama wengine," alisema mama huyo akiwa na mumewe huyo kwa mganga wa jadi Namabengo, wanakopata tiba ya maradhi yanayowasumbua ambayo hawakuyaweka wazi.
Wawili hao ni wakazi wa kijiji cha Lipaya, katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Wakati wenyewe wakijiona kutokuwa na hatia yoyote, jamii imekuwa ikiwazungumzia tofauti, wengi wakilaani uhusiano wao wakisema ni laana. Wakizungumza na gazeti ili juzi Namabengo wilayani Namtumbo, baadhi ya watu waliitaka Serikali ichukue hatua kali za kisheria kukomesha wenye tabia hiyo.
Miongoni mwao, Vailet Gangisa alisema tabia iliyooneshwa na mwanamke mwenzao ni ya kinyama na haipaswi kufumbiwa macho na jamii ya kitanzania, kwani si kitu cha kawaida kwa mtu mwenye akili timamu kufanya mapenzi na mtoto wa kuzaa, achilia mbali kuishi kama mume na mke. Aliishauri Serikali iwapime akili kwanza kabla haijawachukulia hatua, kwa kuwa ni jambo la ajabu na limedhalilisha karibu wanawake wote wa mkoa wa Ruvuma ambao kila wakati wamekuwa wakijitahidi kusimamia maadili ya vijana wao, ili kuepusha vizazi vyao visikumbwe na matukio kama yaliyooneshwa mwanamke huyo.
"Haiwezekani mtu mwenye akili timamu kuishi na mtoto wake kwa miaka hiyo 10 kindoa, ni jambo lililotufedhehesha sana sisi wanawake, sijui huyu mwenzetu amepatwa na pepo gani mbaya hata kumfanya mtoto wake mume! Na kama ni mambo ya kishirikina kwa ajili ya kutafuta utajiri; hivi ni utajiri wa aina gani hadi kujidhalilisha kiasi hicho na mbona bado ni masikini?" Alihoji.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz25EC3al1L