Saturday, September 1, 2012

ASIYE HESABIWA APIGE SIMU SENSA ILI AHESABIWE: MAKAO MAKUU YA TAKWIMU TANZANIA

Kamishna mkuu wa sensa ya watu na makazi Bi Hajjat Mrisho akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Ofisi za Takwimu jijini Dar es Salaam.

Katika zoezi la Sensa lililoanza tarehe 26 Agosti 2012 ambalo lilikuwa limalizike leo limegonga mwamba baada ya kubainika kuwa kuna watu chini ya asilimia tano ambao hawajahesabiwa hivyo Ofisi ya Takwimu kupitia Kamishna wa Sensa  ya watu na makazi amewatangazia watanzania  kuwa zoezi  linaendelea,  kuandikisha watu wote wale ambao hawajaandikishwa hadi tarehe  8 septemba 2012 ili kila mwananchi apate nafasi kwa tathmini iliyofanywa na ofisi ya Sensa.

Kamishna wa Sensa ya watu na Makazi  Bi Hajjat Amina Mrisho amesema kuwa  ili kurahisisha zoezi hilo, anawaomba wananchi wote wale ambao hawajahesabiwa wapige namba zifuatazo ili waweze kuhesabiwa,0222122724,0754583415,0222129622,0713335429.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakiwa kazini