|
Rais wa Rotary Club ya Dar es Salaam Bw Vinay Choudary ( kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha dola 10,000 kwa Mkuu wa hosipitali ya CCBRT Bw, Erwin Telemans ambapo msaada huo ni kwaajili ya kusaidia kununua vifaa vya viungo bandia katika hosipitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam makabidiano hayo yamefanyika leo katika hosipitali hiyo. |
|
Shirika lisilo la kiserikali la Rotary club limekabidhi
Hundi ya dola 10,000 katika hosipitali ya CCBRT kwa ajili ya
kusaidiakutengeneza na kununulia vifaa
vya viungo bandia katika hosipitali hiyo.
Rais wa Rotary club ya Dar es Salaam Bw, Vinay Choudary amesema kuwa
fedha hizo zitasaidia kuhudumia wagonjwa
150 Pamoja na kununulia vifaa katika hosipitali hiyo.
|
Meneja Kitengo cha Viungo bandia Bw, Maunice Rondo kulia akifafanua mbele ya wadau wa Rotary Club ya Dar es Salaam namna ya mguu wa Bandia unavyotengenezwa na kutumia. |
|
Hapa anaonyesha moja ya idhaa inayotengenezwa katika hosipitali hiyo |
|
Fundi akiwa kazini kutengeneza mguu wa Bandia |