Rais wa Chama cha walimu Tanzania CWT akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya chama hicho ambapo amesema kuwa,
anawapongeza walimu kwa kutii amri ya kutekeleza
mgomo na amesema kuwa walimu wasiogoma ni wasaliti, wanafiki na wanasubiri
kupata haki zao kwa kupitia mgongo wa wenzao.
Aidha walimu wametakiwa kuendelea kubaki nyumbani na
wasiende shule kwani wataonekana kuwa ni wasaliti na watasingiziwa kuwa
wanawatumia wanafunzi kuandamana.
Aliongeza kuwa kwa baadhi ya viongozi(wakuu wa mikoa)
wanaosema kuwa mgomo si halali hawana haki ya kusema hivyo kwani watakaosema
kuwa mgomo si halali ni Mahakama
Aliongeza kuwa Chama kinatoa wito kwa serikali kuwa iwaachie huru walimu
Tanzania CWT waliokamatwa na polisi na
wale waliofunguliwa katika Wilaya ya Tarime, Rungwe, Kyela, Babati na sehemu
zingine.
Pia amewataka wakuu wa mikoa waache kutumia madaraka yaokwa
kuwatisha viongozi wa chama cha walimu kwakuwa wao sio Mwajiri wa walimu na
mgogoro unahusiana na maslahi ya walimu na Mwajiri wao.
Aidha alisema kuwa vitisho vya dola havitasaidia kitu katika
mgogoro huo.
|