Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi ,
inayo chapisha
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akiongea na Waandishi wa
habari katika Ofisi za Kampuni hiyo juu ya malalamiko yake kwa
serikali kutokana na kufungiwa kwa gazeti lake la Mwana halisi jana
ambapo alilaani vikali uamuzi huo uliochukuliwa na serikali na hivyo
kuitaka serikali kufuta mara moja Tamko lake, aliongeza kuwa wao hawana kosa walilo fanya kwani wao wamewajulisha watanzania kile wanachotakiwa kuhabarishwa. Alisema kuhusu kuchapisha habari za Aliyemteka Dk Ulimboka kuwa wao wametafuta mtu aliyewasiliana na Dk Ulimboka kabla ya Tukio na wakawahabarisha watanzania na hivyo wakaitaka setrikali kufuta mara moja tamko lake kwani kuna watanzania waliokuwa wanategemea kula kutokana na Gazeti hilo kwa hivyo kulifungia ni kukaribisha umasikini. Kushoto ni Mhariri wa
Gazeti hilo Bw, Jabir Idrissa. |