Waziri wa
Miundmbinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (CUF) Hamad
Masoud, amejiuzulu wazifa wake kufuatia
ajali ya boti ya MV Skagit, iliyotokea zanzibar hivi karibuni na kusababisha
watu kadhaa kupoteza maisha. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ameridhika kwa kujiuzulu
kwa Waziri huyo na tayari amemteua Rashid Seif Selemani (Ziwani CUF) kushika
nafasi hiyo. Wakati huohuo Makamu wa pili wa Rais wa Serikali hiyo Balozi Seif
Ally Iddi amesema kuwa uamuzi wa kujiuzulu Hamad ni wake binafsi.
|