Majambazi hao waliokuwa wanatupiana risasi na askari amabapo
majibizano yalidumu kwa takriban saa mbili walitokea maeneo ya Barabara
inayotoka Posta kuelekea Buguruni wakiwa na gari ndogo aina ya Saloon yenye
namba za usajili T 169 AKM walikuwa wanafwata na Defender ya Polisi.
Baada ya majibizano hayo Majambazi waliishiwa nguvu baada ya
kuishiwa risasi na hatimae Polisi wakawakamata wakiwa wane na wote wanaume.
Bunduki inasumbua kidogo na mwenzake anaangalia usalama , wakati huo Majambazi waliokuwa wamejificha ndani katika nyumba iliyopo pembeni kidogo na askari hao. |
Hapa Bunduki imekwama sasa anakwenda kubadilisha |
Tayari ameipata nyingine kwahiyo ni kazi mwendo mmoja |
Defender moja ya polisi iliyokuwemo maeneo hayo |
Askari akiangalia usalama akiwa kwenye Gari lao |
Askari walimwagika balaa na ilikuwa ni shughuli nzito |
Hapa wanasubiri kama majambazi watasalimu Amri. |
Hili gari limewahifadhi majambazi wawili ambao wanalindwa na askari baada ya kufanikiwa kuwakamata ikiwa bado kuna majambazi wengine ambao bado hawajatoka ndani na wanaendelea kupiga risasi juu . |
Moja ya Jambazi aliyekamatwa na askari hao na nyumba yenye geti jekundu ndimo ambapo majambazi hao walikuwa wamejificha. |
Hili ni gari ambalo majambazi hao walikuwa wanalitumia. |