Saturday, July 7, 2012

WAWILI WAJERUIWA KWA KUPIGWA RISASI KATA YA MABWEPANDE


Mwenyekiti  wa kijiji Cha Kinondo Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni  Bw, Jastin Frenk  akiongea na waandisshi wa habari juu ya mkasa uliowakumba kijijini Kwao baada ya Kuvamiwa na Kupigwa Risasi na Mwanakijiji mwenzao aliyetambulika kwa jina moja la Mwamaso.
Akizungumza na Waandishi wa habari Bw, Justin alisema kuwa tukio hio lilitokea Jumatano ya wiki hii majira ya saa nne asubuhi, ambapo Bw, Mwamaso alikuja kijijini na kuwakuta watu wapo shambani wanafanya usafi na kuanza kuwafyatulia risasi.

Alisema kuwa  Sababu za kufyatua Risasi ni Mgogoro wa Ardhi, wanadai kwamba  Mwamaso amevamia eneo lao na kuingiza tingatinga kwa madhumuni ya kulima na kudai kuwa hilo eneo ni lake.

Aliendelea kusema kuwa , baada ya kumuona Mwamaso anawafyatulia Risasi walimtaka aache  na waonyeshe Mpaka wa eneo lake na la wanakijiji  hicho  lakini Mwamaso hakutaka na aliendelea kufyatua risasi na matokeo yake aliwajerui watu wawili na kuwavunja Mguu.

MAASINDA iliwatafuta Majerui hao waliopelekwa katika hosipitali ya Mwananyamala na kufanikiwa kuonana na Majerui Mmoja aliyetambulika kwa jina la Juhudi Leornad ambaye alidai kuwa yeye alikuwa Mpita njia na Risasi ilimpata akiwa anapita.
“Mimi nilikuwa, napita tu lakini nashangaa nilipigwa risasi na nikaumizwa mguu nikapelekwa Hosipitali ya Mwananyamala na kwa bahati mbaya Mwananyamala wakashindwa kunihudumia ikabidi wanipeleke muhimbili ndipo tulipopata matibabu mimi na Mwenzangu ambapo mpaka sasa Mwnzangu amelazwa Muhimbili  kutokana na hali mbaya ya Mguu wake” Alisema Juhudi.
Aidha MAASINDA ilijaribu kumtafuta Mwamaso lakini hakupatikana kutokana na simu zake zote za mkononi kutopatikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa KIpolisi Kinondoni Charles Kenyela alipoulizwa kuhusiana na swala hili alisema kuwa atatoa taarifa rasmi siku ya Jumatatu kwani alikuwa bado analifanyia uchunguzi.

Bw, Justin Frank akionyesha  Baadhi ya maeneo yanayomilikiwa na Bw, Huyo aliyefahamika kwajina moja la Mwamaso ambapo alisema kuwa anamiliki zaidi ya Hekta Miamoja. 
 Mmoja wa Majerui aliyejeruhiwa na Risasi Bw,Juhudi Leornard akionyesha Jeraha lake kwa waandishi wa habari.
 Bw, Juhudi akijaribu kusimama kwa shida alikokuwa amekaa.

Hiki ndicho kidonda cha Juhudi.