Saturday, July 7, 2012

MBELGIJI WA YANGA ASAIN MKATABA

Kocha mpya wa Yanga, Thom Saintfiet jioni hii amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu hiyo na baada ya kusaini, akasema hakuja Tanzania ‘kustarehe’ amekuja kufanya kazi na sera yake ni ushindi. Anataka ushindi na mataji. Amesema jaribio lake la kwanza ni kutetea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, katika michuano inayoanza Julai 14, Dare s Salaam (Habari kamili baadaye). Tazama picha za kusaini kwake Mkataba makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.