Wednesday, July 4, 2012

WATANZANIA WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO ILI KUJUA KAMA WAMEATHIRIKA NA KISUKARI

Katibu wa Chama cha Kisukari Tanzania Dk Kaushik Ramaiya akiongea na waandishi wa Habari leo hii katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa wadau wa kisukari nchini  waliokutana  kuwasilisha  Takwimu za wagonjwa wa Kisukari nchini ambapo alisema kuwa katika watanzania mia waishio mijini waliopimwa walikuwa kuna wagonjwa nane wa Kisukari na hivyo aliwataka watanzania kupima na kujua afya zao mapema ili waweze kupata tiba. Aidha Dk Ramaiya alisema kuwa anaiomba serikali iboreshe huduma za kutolea tiba kwa wagonjwa wa Kisukari akatika hosipitali zote nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha kisukari Tanzania Bw,Ramadhani Mongi, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari waliokuwemo kwenye mkutano huo ambapo alisema kuwa ni vyema kwa Watanzania kupunguza kunywa vinywaji vyenye ulevi ili kupunguza idadi ya wagonjwa wa kisukari Nchini.Aidha Bw Mongi aliwataka walioathirika na Kisukari kuwa na Mazoea ya kufanya Mazoezi kila siku ili waweze kuishi miaka mingi.