Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe, Khamis Kagasheki (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusu
Kamati ya Urithi
wa Dunia ya UNESCO katika kikao chake cha 36 kinachoendelea (tarehe 24 June
hadi 6 Julai 2012) katika jiji la Saint Petersburg nchini Russia kuwa imelikubali
ombi la Tanzania la kuurekebisha mpaka wa Pori la Akiba la Selous, ambalo ni
Eneo la Urithi wa Dunia, ili kuruhusu uchimbaji wa Madini ya Urani. Eneo
linalohusika ni asilimia 0.8 ya eneo la
Pori la Akiba la Selous. Kagasheki alisema kuwa,
Kwa mara ya
kwanza ombi hilo lilipelekwa kwa Kamati hiyo
ya Urithi wa Dunia ya UNESCO mwezi Januari 2011 ambapo lilijadiliwa katika
Kikao chake cha 35 ambacho kilihamishia mjadala huo katika Kikao cha 36 kinachoendelea. Uamuzi huo
ulifanyika ili kuruhusu Tathmini ya Athari ya Mazingira (EIA) kukamilishwa na kutoa
muda kwa wataalam wa IUCN kufika eneo linalihusika ili kuliona na kuhakiki
taarifa ya tathmini hiyo.
|