Monday, July 23, 2012

WASANII WTAKIWA KUWASHIRIKISHA WATOTO WA SHULE KATIKA SANAA

Mkurugenzi wa Ngoma Africa akitoa mada katika jukwaa la Sanaa lililofanyika katika makao makuu ya Baraza la Sanaa jijini Dar es Salaam, Mada ikiwa, Sanaa kwa watoto mashuleni Msingi Imara kwa Maendeleo ya Tanzania 
 Wasanii wametakiwa  kuwashirikisha watoto katika kazi za sanaa kwa ajili ya kukuza Sanaa kwa kizazi kijacho.
Akizungumza wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika Kwenye  ukumbi wa makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa Basata, mkurugenzi wa  kampuni  ya sanaa za maonyesho Ngoma Afrika Bw, Davie Kitururu , alisema kuwa moja ya Changamoto inayowakumba wasanii wachanga ni utayari wa wasanii wakubwa kutotenga muda wa kushirikiana na watoto katika sanaa.

Kitururu amewaomba wasanii kutenga hata angalau saa moja kwa ajili ya kuwahamasisha watoto Shuleni  juu ya umuhimu wa sanaa.
Aliwataka wasanii pia kujitambua kwamba wao ni kioo cha jamii na  kuvaa mavazi ya kiheshima illi kujenga taifa lenye maadili mema.
“Msanii wa kiafrika hatakiwi kuvalia suruali Matakoni au wanawake kuvaa nusu uchi na kuacha mapaja yao wazi huo sio usanii wala sio kioo cha jamii kwa mwendo huu tutakosa Tanzania yenye maadili mema kwani watoto wakiona hivyo wanaiga kila kitu” alisema Kitororo.
Katikati ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Sanaa Bi, Nsao Shalua Kushoto ni Mkurugenzi wa  Kampuni ya Sanaa za Maonyesho (NGOMA AFRIKA) yenye ofisi zake mjini Morogoro na wamwisho kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Sanaa Bi, Elineea Ndowo. 

Baadhi ya wadau wa sanaa wakisikiliza kwa makini.