CHAMA cha walimu
Tanzania (CWT ) kimeitaka serikali kushughulikia madai yao kabla wao
hawajafikiria kuchukua hatua nyingine
ambapo alisema kuwa ikiwa
serikali itashindwa kuwasuluhisha Chama kitawatangazia wanachama wake juu ya Uamuzi wao wa kupiga kura ambapo walimu watajulishwa tarehe ya kupiga kura
ili kuamua kuhusu walimu kugoma
au kutogoma . Alisema kuwa ikiwa
kura zitapigwa na walimu wengi wakaunga mkono mgomo , Chama cha walimu
Tanzania CWT kitaitisha kikao cha dharura
cha Baraza la Taifa kuamua juu ya
aina ya Mgomo na muda wa Mgomo kama inavyoelezwa kwenye
nyaraka za (CWT).
Aidha alisema kuwa
endapo kutakuwa na mgomo taarifa itatolewa na Rais wa CWT na sio kiongozi mwingine yeyote wa Chama.
|