Chama cha
walimu nchini Tanzania (CWT) Kimeitangazia serikali kuwepo na harufu ya Mgomo
ambao imeanza kunukia baada ya serikali
kushindwa kusuluhisha mgogoro wake na walimu.Rais wa Chama cha walimu Gratian
Mukoba amesema leo katika makao makuu ya Chama cha walimu jijini Datr es Salaam
wakati akiongea na waandishi wa habari kuwa, Tarehe 25 julai saa 4 Asubuhi CWT Na
serikali zilifika mbele ya Msuluhishi kupewa cheti cha kuonyesha kuwa Usuluhishi umeshindikana . Ambapo kwa maelezo
hayo CWT kiliwaagiza walimu kuanza kupiga kura baada ya kupewa cheti hicho, ambacho ni kama Kibali cha wao kugoma.
Mukoba alisema kuwa zoezi la walimu kupiga kura litaendelea mpaka kesho Asubuhi
na baada ya muda huo kupita Chama kitapokea matokeo kutoka kila wilaya na Endapo
kura za ndio zitakuwa nyingi mgomo utaanza kabla ya Zoezi la Sensa.
Aidha Mukoba
alisema kuwa mgomo wa walimu hauna Mahusiano na zoezi la uesabuji watu
(Sensa) kwa hivyo walimu watashiriki
katika sensa kama kawaida na Mgomo utakuwa palepale.
|