Rais Mpya wa Ghana John Dramani akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo.
Kwa hisani ya Mtandao
Kiongozi mpya wa Ghana John Dramani Mahama, ameahidi kuimarisha hali
ya utulivu kufuatia kifo cha Rais John Atta Mills. Bw. Mahama mwenye umri wa
miaka 53, aliapishwa saa kadhaa baada ya Rais aliyekuwa na umri wa miaka 68
kufariki hospitalini mjini Accra.
Upinzani
wa nchini humo umesifu kasi iliyotumiwa katika kufanya mabadiliko
yaliyomkabidhi Bw.Mahama mamlaka ya kuiongoza nchi ya Ghana na kusema kuwa ni
kuonyesha kuwa Ghana ina upevu Kidemokrasi.Bw. Atta Mills aliyeiongoza Ghana
kuanzia mwaka 2009 alikua na saratani ya koo na alikua na mipango ya kuwania
muhula wa pili katika uchaguzi unaopangwa kufanyika mwezi disemba.
Mwandishi wa BBC mjini Accra, Sammy
Darko anasema kuwa Rais aliyekabidhiwa wadhifa wa Rais ataongoza kama Rais hadi
wakati wa uchaguzi, ingawa haijafahamika kama atasimama kama mgombea rasmi wa
chama cha NDC(National Democratic Congress.)Wakati wa kuapishwa mbele ya kikao
maalum cha Bunge kilichoitishwa kwa dharura, Bw.Mahama aliahidi kuwahudumia
raia wote wa Ghana. Punde baada ya kutangazwa kuwa Rais, Bw.Mahama alitangaza
maombolezi ya wiki nzima.
Kiongozi wa upinzani wa chama cha
New Patriotic Party Nana Akufo Addo amesema ameahirisha kampeni za kugombea
kiti cha Rais kwa heshima ya marehemu.Mwenyekiti wa NPP Jake Obetsebi-Lamptey
amesifu jinsi mabadiliko yalivyofanywa kufuatia kifo cha Rais.Ingawa kulikuepo
na mjadala mkubwa kuhusu afya ya Bw.Atta Mills, suala hilo halikugusiwa rasmi,
wanaserma wandishi wa habari. Kiongozi huyo alikanusha kuhusu maumivu na
kusisitiza kua katika hali nzuri ya afya.
Kulingana na msaidizi wa Rais,
marehemu alilalamika kua na maumivu siku ya jumatatu jioni na tangu hapo hali
yake ikazidi kua mbaya.
|