Chama cha walimu kimeitangazia Serikali kuwa Mgomo wake
unaanza Rasmi siku ya Jumatatu baada ya kura zilizopigwa na walimu kuonekana
kuwa asilimia 95.7 ya wanachama wameunga mkono Mgomo . Raisi wa Chama cha
Walimu Tanzania CWT Bw, Gratian Mukoba amesema
leo wakati akiongea na waandishi wa habari kuwa, walimu waliopiga kura ni,
Walimu wa shule za awali, Msingi, Sekondari, maafisa waliopo kwenye ukaguzi
wa shule na wakufunzi wa vyuo vya ualimu
na maendeleo ya Jamii.
Alisema kuwa Mgomo
huo umeungwa mkono na walimu Takriban 153,848 ambapo ni zaidi ya nusu ya
wanachama wote waliopiga kura. Kwa hivyo Baraza la CWT limetoa notisi ya saa 48
kwa serikali kuanzia jana tarehe 27
julai saa nane mchana na baada ya saa hizo walimu wataanza mgomo wa kubaki
nyumbani bila kwenda kazini kuanzia siku
ya Jumatatu tarehe 30 julai 2012 hadi
hapo watakapo arifiwa na Rais wa CWT Bw, Gratian Mukoba.
Mukoba aliwataka walimu kushiriki Mgomo huo ambao ni
halali ambao umeitishwa na chama kwa mujibu wa Sheria.
|