Baadhi ya Wakufuzi wa Sensa waliohudhuria katika ufunguzi wa mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 ngazi ya Mkoa wakimsikiliza mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh, Said Meck Sadick.Katika ufunguzi huo Mkuu wa mkoa aliwataka
Viongozi wa Vyama na Serikali katika ngazi zote kwa
ujumla kutoa ushirikiano katika kuhamasisha na kuelimisha umma
umuhimu wa kushirikiana na makarani wa sense kwa kutoa taarifa sahihi wakati wa
zoezi la kuhesabu watu.
Akihutubia wakati wa kufungua mafunzo ya wakufunzi
wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam leo,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amewakumbusha wananchi
kwamba shughuli zao za kiuchumi na kijamii hazitakwamishwa na zoezi la sense
litakalochukua siku zisizozidi saba.
Aidha amewahakikishia wananchi kuwa taarifa
zitakazokusanywa zitatumika kwa Siri na zitatumika kwa shughuli za kitakwimu
tu, kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2002.
|