Mkurugenzi
wa Global Publishers, Bw, Erick Shigongo
ambaye alikuwa analalamikiwa na Mwanamuziki Jose Chamilione kuwa amechukua
Pasport yake ya kusafiria amewataka Wasanii kuacha tofauti zao katika kutetea
maslahi ya nchi na si vinginevyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana, na Mkurugenzi huyo alipokuwa akizungumza na wandishi
wa habari kuhusu kuzulumiwa dola 3500 na msanii wa Uganda Jose Chameleone.
Alisema
ameshangazwa na baadhi ya Watanzania kumchafua kwenye mitandao kwa kitendo
chake cha kumdai msanii huyo wa Uganda, fedha walizokubaliana katika mkataba
ili kufanya onyesho la Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Shigongo
alisema huu ni wakati kwa watanzania kufahamu ukweli kuhusu hilo kutokana na
ukweli kwamba msanii huyo, amekiuka makubaliano ya mkataba wa kwanza ambao
walikubaliana kufanya onyesho hilo ghafla akageuka kudai fedha zaidi.
Alisema
hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikubali kuingia mkataba mwingine kwa mara ya pili
kutokana na ukweli kwamba alikwishafanya matngazo kuwa msanii huyo angekua
mmoja wa wasanii ambao wangefanya onyesho katika tamasha hilo.
“Kweli
tulikubaliana mkataba mwingine nikamlipa dola 8000 na kweli alikuja akafanya
onyesho lakini baada ya hapo ndipo nilipomdai fedha zangu dola 3500 alizochukua
katika makubaliano ya awali”alisema Shigongo.
Shigongo
alisema si kweli kwamba alizuia pasipoti ya msanii huyo wakati alipokuwa
amepangisha chumba kwenye hoteli yake bali kilichotokea ni msanii huyo kuondoka
mwenyewe baada ya kudaiwa fedha hizo.
Katika
hatua nyingine, Shigongo alisikitishwa na kitendo cha msanii huyo akishirikiana
na vijana wenzake kuvamia ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kwa madai ya kudai
kurudishiwa pasipoti yake.
|