Monday, July 2, 2012

POLISI WAKAMATA WALIOIBA TCU

Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na namna ya  Jeshi la la polisi Mkoa wa Kinondoni lilivyojitahidi kuwakamata wahalifu mbalimbali waliojihusisha na matukio tofauti likiwemo lile la Kuiba na kufanya uharibifu katika ofisi za Tume ya Vyuo vikuu  (TCU) ambapo alisema kuwa wamewakamata Majambazi 7 na alitaja baadhi ya Vitu walivyokamatwa navyo ni, Nyaraka Mbalimbali za TCU Vitabu vya hundi pamoja na Funguo zas Magari. Aidha walifanikiwa kukamata Gari aina ya Noah lenye namba za Usajili T.885 CAK.

    
Kamanda Kenyela akionyesha Gari aina ya NOAH lililoka
matwa katika tukio hilo

Namba za usajili la Gari hilo ambapo kamanda Kenyela alisema kuwa  gari hili lilitumika katika Tukio la wi zi lililofanyika katika tume ya Vyuo Vikuu  (TCU).

Kamanda Kenyela akionyesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kutokana na Msako uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni vifaa hivyo ni TV kubwa,Redio, pamoja na Computer Mbalimbali.