Mkuu wa Polisi wilaya ya Kinondoni Bw, Wilbord Mutafungwa akiongea na wawakilishi wa michezo kutoka kata zote za Wilaya ya Kinondoni juu ya namna ya Kuimarisha Michezo katika wilaya hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa Michuano ya Polisi Jamii Cup uliofanyika katika Kiwanja cha Polisi Ostabey Jijini Dar es Salaam. Kamanda Mutafungwa alisema kuwa michuano hiyo inatarajiwa kuanza hivi karibuni na lengo la michuano hiyo ni wananchi kujenga urafiki na polisi kwa makusudi ya kukomesha uhalifu katika wilaya ya Kinondoni. Alisema kuwa katika michuano hiyo kutakuwa na walimu maalum wa kufundisha vijana athari za uhalifu ambapo alisema kuwa katika mashindano hayo mshindi atapndoka na kitita cha shilingi milioni moja. |