Tuesday, July 3, 2012

HAMNA FUJO WALA MGOMO KATIKA HOSIPITALI YA MWANANYAMALA

Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela akifafanua jambo kwa mwandishi wa Habari  baada ya kufika katika hosipitali ya Mwananyamala kutoka na uvumi uliojitokeza kuwa Madaktari wa Hosipitali ya Mwananyamala wanafanyiwa Fujo na ndugu wa wagonjwa jambo ambalo lilionekana kuwa ni uvumi baada ya askari kufika pale na kukuta huduma zinaendelea kama kawaida. Kamanda kenyela alisema kuwa Hamna fujo wala dalili yoyote ya Fujo na Huduma zinaendelea hosipitalini kama kawaida.





Kamanda Kenyela na mwandishi wa habari wakifurahia jambo hosipitalini hapo.

Katibu wa Madaktari hosipitali ya Mwananyamala  Bw, Eduin Bisakala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na uvumi wa Fujo uliovuma kuwa katika hosipitali hiyo kuna vurugu.Bisakala aliwataka wananchi waende kupata huduma katika hosipitali hiyo kwana Madaktari wa hosipitali hiyo hawajagoma.

OCD wa kinondoni  akiwa hosipitalini hapo kuhakikisha kuwa amani inakuwepo.

Ma Afisa wa polisi wakiwa hosipitalini hapo.