Mjumbe wa Kijiji cha Nyakasangwe, Jastin Frank, akisisitiza jambo kuwa hawawezi kukubali kunyanyaswa na polisi wanaotokea kuwanyanyasa hapo kijijini kwao wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam. |
Katibu mwenezi wa CCM, Tawi la Nyakasangwe Bw, Benjamin Steven akisistiza jambo wakati alipokuwa akiongea naWaandishi wa habari juu ya unyanyasaji wao dhidi ya Polisi. |
Wanakijiji wa Nyakasangwe Kata ya Wazo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wanaiomba serikali iwaangalie na kuwasaidia
kuondokana na unyanyasaji wanaoupata Dhidi
ya Polisi wa kupigwa pamoja kufukuzwa katika maeneo yao huku wakiwaambia kuwa wao ni wavamizi katika
maeneo hayo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kijijini hapo
wanakijiji hao walisema kuwa wamechoka kuishi kwa kunyanyaswa na polisi bila ya
makosa yoyote kwani wanaishi kama digidigi (pasipo kulala) na Kisingizio cha
wao kunyanyaswa ni kwamba hawatakiwi
kuishi kwenye maeneo hayo kwakuwa wao si wamiliki halali.
Majengo
Majengo ni Mwenyekiti wa kijiji hicho ambapo alisema kuwa Polisi wanakuja kila
kukicha kutaka kuwakamata kwa kisingizio kwamba wanakijiji wote wanaoishi
maeneo yale ni wavamizi.
Hata hivyo
Majengo alisema kuwa, Kesi yao ipo mahakamani na inasubiriwa kutolewa hukumu
lakini wanashangaa bado wanakamatwa ovyo na kubambikiwa kesi.
“Kesi yetu
hii ipo mahakamani lakini tunashangaa tunazidi kuwindwa na watu wachache,
wakishirikiana na Polisi”,alisema Majengo.
Alisema
kuwa, Askari hao wanapokwenda kuwakamata, wanatembea na watu watatu wanaodai kuwa msitu wa kijiji hicho ni maeneo yao.
Aliwataja
watu hao kuwa ni,Datsan Okololo, Omary Ponchi pamoja aliefahamika kwa jina moja
tu la Mwamasika ambao alidai kuwa ndio
wanaoshirikiana na askari wa jeshi la polisi kuwakamata watu kwa madai ya kuwa
wao ndio wamiliki halali wa msitu huo wa kijiji hicho.
Naye Katibu
Mwenezi wa CCM Tawi Nyakasangwe Benjamin Steven, alisema
kuwa viongozi wenzake wote wamekamatwa
na polisi na Mpaka sasa Mwenyekiti wake hajulikani alipo baada ya kukimbia
askari walipotaka kumkamata.
Akielezea kukamatwa
huko kwa viongozi wenzake alisema kuwa,
baada ya uchaguzi uliofanyika
tarehe tano mwezi huu yalikuja magari mawili ya polisi(Defender)
zilizofunikwa na vitambaa vyeusi kwenye
ubao wa namba na kuwakamata viongozi wao kwa makosa ya Uvamizi.
“Mimi nashangaa
Maswala ya Uvamizi yanaingiliana vipi na Chama, naomba jeshi la Polisi
lisichanganye mambo, kwa mambo ya Uvamizi yanamuhusu mwenyekiti wa kijiji na
serikali yake na hayawezi kuhusiana na Chama hata siku moja”, alisema Benjamin
Steven.
Hata hivyo Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimana
alipoulizwa kuhusiana na sakata hili alisema kuwa kuhusiana na wannchi hao
kunynyaswa na kubomolewa nyumba zao kwa kosa la uvamizi ni swala la Mahakama ndiyo itakayotoa majibu kama wanakijiji hao
wanauhalali wa kuishi maeneo hayo au la.
Aidha, kamanda
wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alipoulizwa kuhusiana na
swala hilo alisema kuwa, huo ni mkakati wa jeshi la polisi kuendelea kuwakamata
wavamizi wa maeneo ya watu.