BENDI zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na
Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya
Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana ukumbi
wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay
Entertainment, Paul Maganga walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na
kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema siku
hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza
kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila
mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya
utamaduni wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine na burudani
kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine vya
ngoma ya asili ” alisema Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa mila ambo
watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili
kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo,
ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema baada ya Tamasha la hilo la
‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro,
Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha
haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua
mila zao sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa
kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina
ya makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata
kujua chimbuko la kuweko kwa tamaduni zao yaani mashujaa wa
makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni
pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro, SBC Tanzania (Pepsi),
Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC
Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant,
Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata
Decorations.
|