Tuesday, July 10, 2012

MASHINDANO YA KUWANIA KIKOMBE CHA POLISI JAMII YAANZA RASMI JIJINI DAR

Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akitoa nasaha kwa vijana mbali mbali wa wilaya hiyo wakati wa ufunguzi wa michuano ya polisi Jamii wilaya ya Kinondoni, wanaonsikiliza kwa makani ni Rpc wa Kinondoni Charles Kenyela(kushoto) na mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Willbroad Mutafungwa(mwenye sare za polisi)Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa polisi wilaya ya Kinondoni Kamanda Willbord Mutafungwa akisema jambo wakati wa wa ufunguzi  wa michuano ya polisi Jamii wilaya ya Kinondoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akiwa hana la kufanya baada ya kushindwa kudaka mpira uliopigwa na mkuu wa polisi katika wilaya ya Polisi Kinondoni Willbroad Mutafungwa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa michuano ya Polisi jamii katika wilaya hiyo ambapo timu 12 za kata nane zinawania ubingwa na zawadi ya ushindi wa kwanza wa shilingi milioni moja

Baadhi ya timu zilizoshiriki katika michuano ya Polisi  Jamii Cup  wakipata wosia kutoka kwa viongozi waliovalia jezi za njano ni wachezaji kutoka Kinondoni Muslim ambapo waliwashinda wenzao kutoka mwenge kwa Magoli kumi na Moja kwa Moja.Mshindi katika fainali za michuano hiyo ataondoka na kikombe pamoja na Fedha Taslim shilingi Milioni Mbili za Kitanzania.