Sunday, July 8, 2012

CHADEMA WASTUKIA KWAMBA VIONGOZI WAO WANATAKA KUFANYWA ALICHOFANYWA DK ULIMBOKA, WASEMA WAMEWASTUKIA USALAMA WA TAIFA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo   CHADEMA na Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti  wa Kambi ya Upinzani  Mhe Freeman Mbowe, akiongea na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam kuhusiana na Usalama wa Taifa kuwafwatilia viongozi  wa Chama hicho kwa Vitisho vya kuwadhuru,  alisema kuwa  Usalama wa taifa unawafwatilia baadhi ya viongozi wa CHADEMA  kwa masaa ishirini na nne na kuongeza kuwa wanataka kuwadhuru. Aliwataja  viongozi wanaofwatiliwa na Usalama wa Taifa kuwa ni John Mnyika  Mbunge wa Ubungo, Godbless lema  aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini  Pamoja na Dk Wilbord Slaa katibu mkuu wa Chama hicho ambapo walisema kuwa tayari wamewagundua watu wanaowafwatilia  na akawataja kwa jina moja moja kuwa ni Rama, na Zoka ambao wanawafwatilia viongozi hao kila waendapo.


Mbunge wa Ubungo John Mnyika akielezea namna anavyofatiliwa na Usalama wa Taifa na kusema kuwa amepata taarifa kutoka kwa vyanzo vyao  vya habari kuwa anafatiliwa na wanaomfwatilia wanampango wa kumuwekea sumu au kumtesa. Aliongeza kuwa pamoja na hayo yote yeye haogopi na ataendelea kufanya  kama alivyotumwa na wananchi.
“Kama ni uhai Mungu ndo ametupa kwa hivyo yeye ndo anauwezo wa kuuchukua uhai wangu mimi siogopi chochote na nitaendelea kuwasema mafisadi ili jamii ijue ukweli” alisema Mnyika. Aidja alisema kuwa tayari amewaeleza wazazi wake kuhusiana na vitisho hivyo na akaambiwa aendelee kutetea wananchi na kupewa Baraka zote na wazazi.

Dk Slaa akielezea namna anavyofwatiliwa ambapo alikumbushia namna alivyowekewa vinasa sauti kwenye chumba chake n a mpaka leo akiuliza ni nini am,bacho kilikuwepo kwenye hivyo vinasa sauti hapati jibu hivyo akasema kuwa Zoka atambue kuwa Tayari chadema wamegundua vitu anavyo vifanya.

Lema naye akielezea namna anavyofatiliwa na kusema kuwa  kuna gari linalao mfwatilia kila anakoenda na jana tu alikuwa anatoka Serena  hotel  alisema kuwa haogopi na bado ataendelea kuwatetea wananchi.