Saturday, July 28, 2012

MACHANGUDOA WAPEWA KICHAPO NA WAISLAMU KATIKA PITAPITA ZA MWEZI MTUKUFU

Changudoa aliyekutwa na Kiboko cha Shehe kutoka kikundi cha Uamsho cha Tanzania Bara akiomba msamaha.Masheikh hao waliamua kuzunguka sehemu mbalimbali ambazo biashara ya Uchangudoa imetawala hapa jijini Dar es Salaam na kisa cha wao kufanya hivyo wanadai Machangudoa hao wanawaharibia swaumu kwenye kipindi hichi cha mwezi mtukufu.

Kikundi hicho cha uamsho kilianzia Maeneo ya Sinza na ndiko walikofanikiwa kuwakuta Makahaba wengi


Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.

Changudoa akikimbia baada ya kuona kimemnukia

Huyu naye miguu iliota Mbawa