Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe(wapili kutoka kushoto) akiwa kwenye maandalizi ya Tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika mkoani Kigoma. Naye msimamizi wa ama mratibu wa
tamasha hilo Mwasiti Almas(wakwanza kulia) naye alifunguka na kusema haya "Kila kitu
kwetu kama wasanii wa Kigoma kiko tayari kwa ajili ya tamasha hili,
Kilichobaki ni wasanii wenyewe kufika mkoani kwao na kutimiza lengo la
Tamasha hili, kwani tamasha hili linasimama kuwatia chachu ama hamasa
vijana wa mkoa wa Kigoma mkoani humo".
LEKA
DUTIGITE KIGOMA.. ni tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika mkoani
Kigoma tarehe 17 ndani ya mwezi huu wa saba na kuwashwa moto na wasanii
wazawa wa kigoma. Mpaka sasa ari waliyonayo wasanii hao ni ya kubwa
mno.. mpaka imekuwa kama ni changamoto kwa wasanii wanaotoka katika
mikoa mingine, na kulowea zaidi Dar es Salaam.