Temeke imefainikiwa kuilaza Dodoma
mabao 2-0 katika mechi ya kundi C ya michuano ya Copa Coca-Cola iliyochezwa leo
(Julai 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Mabao ya washindi ambao kwa matokeo hayo sasa
wamefikisha pointi tano yalifungwa dakika ya tano Hassan Kabunda wakati la pili
lilifungwa dakika ya 34 na Abdul Hassan.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam umeshuhudia Morogoro ikiibuka
na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Iringa lililofungwa dakika ya 37 na Mutalemwa
Katunzi.
Nayo Kilimanjaro imeibuka na ushindi wa bao 1- dhidi
ya Tabora katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Bao hilo katika mechi hiyo ya
kundi D lilifungwa dakika ya 14 na Eric Christopher.
Kwa matokeo hayo Tabora imebaki na pointi tatu baada
ya kushinda mechi moja tu dhidi ya Pwani, na imebakiza mechi moja dhidi ya
Kusini Unguja ambayo hata ikishinda haiwezi kuingia hatua ya 16 bora.
Nao mabingwa watetezi Kigoma wamejiweka katika nafasi
nzuri ya kucheza 16 bora baada ya kuitandika Kusini Pemba mabao 3-1 katika
mchezo wa kundi A uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko mkoani Pwani.
|