Mkuu wa
jeshi la polisi nchini Uganda, IGP, Kale Kayihura amewaagiza maofisa wa
Tanzania kuirudisha haraka passport ya Jose Chameleone.
Kayihura
ametoa amri hiyo alipokutana na Chameleon kwenye kituo cha polisi cha Muyenga
mchana wa leo jijini Kampala.
Amesema
maafisa wa hapa nchini wamesema passport ya msanii huyo ingewasili baadaye leo
na kukabidhiwa kwake mara moja.
Leo Jose
Chameleone akiwa na mashabiki wake wameandamana kwenye ubalozi wa Tanzania
nchini Uganda kudai arudishiwe passport hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Erick
Shigongo kwa madai kuwa meneja wake amemtapeli dola 3500.
|