Sunday, July 29, 2012

ETI VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA USALAMA WA TAIFA WANAOGOPA KUPATIWA NATIBABU MUHIMBILI

Nikinukuu Jamii Forums ni kwamba, kwa siku za karibuni inaonekana wazi baadhi ya watu na viongozi wa serikali wamekuwa wakigwaya kwenda kutibiwa Muhimbili. Kwa tetesi zilizopo licha ya baadhi ya askari na watu wa usalama wa Taifa kuwa na hofu kubwa kuhusus kupelekwa muhimbili pindi wapatwapo na ajali au kuugua, ina semekana kwamba wengi wa viongozi sasa hasa wa CCM wana kwenda hospitali za binafsi hasa Agakhan na Regency, kwa madaktari wanaowaamini tu! Hii inaonekana ni kwa kile kitendo chao cha kufurahia kupigwa ulimboka na kuwadhihaki madaktari. Pia inaelezwa kwamba sababu nyingine ni hofu kuhusu mgomo baridi unaondelea sasa katika mahospitali yetu, hasa kutokana pia na kufukuzwa baadhi ya madaktari na madaktari wanafunzi kwa kudai maboresho katika sekta ya Afya.

Je hii hali ya kutoamiana kati ya "wagonjwa' na madaktari iliyotengenezwa na serikali itaendelea mpaka lini? Hata wananchi wa kawaida siku hizi huwa hawana imani na tiba wanazopewa hospitalini km kweli ndio best possible ya matibau wanayoweza kupata kutoka kwa madaktari wao! Hii inatokana na kinyongo ambacho bado madaktari wamebaki nacho!

Je serikali inalijua hili na ni nini wanachofanya kuhakikisha watu wa kawaida na viongozi hasa wa CCM wanarudisha imani kwa madaktari wetu? Na ni nini serikali inafanya kuhakikisha wanamaliza kinyongo na manunguniko waliyonayo madaktari ili warudishe moyo wao wa kufanya kazi kwa ufanisi na kujtolea?

Njia ya kutumia nguvu na vyombo vya dola kama mahakama kweli inaweza kurudisha ari, kuaminiana na kujitolea kwa madaktari wetu katikas kuokoa maisha ya watanzania? Tunaomba serikali imalize huu mgogoro na madaktari na washikane mkono na "tuwaone kwenye picha na TV wakicheka" kwa ajili yetu sisi wagonjwa kuturudishia imani hasa na madaktari wetu wa muhimbili ambapo ndipo penye rufaa ya maisha yetu. Imefikia mahali hata ndugu yako akipewa rufaa ya muhimbili roho inakudunda! Tafadhali serikali hebu turudishieni amani ya roho! Tafadhali sana tunaomba sana!