Sunday, July 1, 2012

CWT YASHTUKIA MBINU ZA KUWAGAWA WALIMU

Rais wa Chama Cha walimu  Tanzania CWT Bw,Gratian Mukoba kushoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii ambapo, ametoa wito kwa walimu kuwa macho na baadhi ya watu ambao wanataka kutumia nguvu zao za kisiasa na Fedha, kwa kuwagawa walimu . RMukoba amesema kuwa wanafwatilia kwa karibu taarifa ya kuwepo kwa kikosi kazi, ambacho kimejipanga kuhakikisha kuwa kinawagawa walimu pamoja na kuchochea migogoro ndani ya CWT Kama njia ya kuzima kiu ya Walimu kutaka kudai mishahara yao.

 Aidha, Bw, mukoba alisema kuwa Chama chao kinalaani Vikali unyama aliofanyiwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka ambaye alikuwa anatetea Maslahi ya Madaktari na kutoa wito kwa Tume isiyohusisha Vyombo vya Dola vya hapa nchini kuchunguza kwa makini yaliyomsibu Dk Ulimboka.

Aliongeza kusema kuwa,  Serikali inapaswa kutambua matumizi ya  Nguvu hayawezi kuleta tija Mahali pa kazi.