Saturday, June 30, 2012

POLICE JAMII, KUANZASHA POLICE JAMII CUP

Mratibu Mwandamizi wa Polisi na OCD wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Bw, Wilbrod Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari leo hii Ofisini Kwake jijini dar es Salaam juu ya Uanzishwaji wa mIchuano ya Michezo Mbali mbali kwa walinzi shirikishi wa Mkoa wa Kinondoni inayo Kwenda kwa jina la Police Jamii Cup inayotarajia kuanza hivi Karibuni ambapo alisema kuwa lengo la Michuano hiyo ni Kutoa Elimu kwa jamii juu ya Athari za Uhalifu ambapo kutakuwepo na Semina yenye wataalamu wa kuwafundisha juu ya Athari hizo.
Mratibu Mwandamizi wa Polisi na OCD wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Bw, Wilbrod Mutafungwa kushoto wakikagua baadhi ya Mipira itakayotumika katika michuanao hiyo ambapo alisema kuwa kutakuwe na michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, kufukuza kuku, pamoja na mpira wa Miguu na mshidi katika Michuanop hiyo atajinyakulia Kombe pamoja na Fedha Taslim sh Milioni moja kwa mshindi wa kwanza.