Aliyepanga njama za kutaka
kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na
hatia baada ya mahakama ya Pretoria kumpata kiongozi kutoka kundi la Boeremag ambapo ilimtaja mtu huyo kuwa ni Bw, Mike Du Toit kuwa alipanga njama za kumuua Mandela Mwaka 2002.
Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga
milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.
Kiongozi huyo wa kundi la kibaguzi
ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa viongozi wengi uanze mwaka 1994
Afrika kusini.
Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna
hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.
Hata hivyo kundi kama la
Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi
mkubwa.
Mahakama hiyo ya Pretoria imempata
Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.
|