Tuesday, July 10, 2012

AKILI YA WAZIRI PINDA IMEGANDA: DK SLAA


Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk Willbord Slaa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya Chama hicho  ambapo alisema kuwa akili ya Waziri mkuu Mizengo Pinda imeganda kutokana na Waziri mkuu kusema kuwa CHADEMA haioni kitu ambacho serikali imefanya.Waziri Pinda aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara yake Mkoani Ruvuma na hivyo Dk Slaa akamtaka atambue kuwa CHADEMA wanadai mabaki ya wananchi yaliyopo kwenye MEREMETA,EPA,pamoja na RADA."Waziri mkuu anaposema  CHADEMA hatuoni yaliyofanywa na Serikali inaonyesha dhairi kuwa akili yake imeganda ndio maana anashindwa kufikiri kwamba tunachodai sisi ni Chenji ya wananchi" alisema Dk Slaa. Aliongelea pia swala la kutakiwa kuwadhuru baadhi ya viongozi wa chadema na kusema kuwa Mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA imelaani vikali mpango huo aliodai kuwa umepangwa na Usalama wa Taifa. Dk Slaa aliongezea pia kuwa kuhusu uchunguzi wa polisi kufuatilia swala lao hana imani nao kwani kuanzia alipowekewa vinasa sauti kwenye chumba alichokuwa analala mpaka leo polisi hawajasema chochote.