Friday, June 8, 2012

WAZIRI WA AFYA AELEZEA SIKU YA MAADHIMISHO YA KUCHANGIA DAMU

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Mwezi huu. Uchangia damu wa hiari umeongezeka toka chupa 52,000 kwa mwaka 2005 na kufikia  chupa 140,000 kwa mwaka 2011, kauli mbiu ya mwaka huu ni “kila mchangia damu ni shujaa”.  Kulia ni Naibu Waziri Dk. Seif Rashid

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu  maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Mwezi huu. Uchangia damu wa hiari umeongezeka toka chupa 52,000 kwa mwaka 2005 na kufikia  chupa 140,000 kwa mwaka 2011, kauli mbiu ya mwaka huu ni “kila mchangia damu ni shujaa