Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna wa Tume ya Utumishi wa
Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage
(kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama
kuu kanda ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
akifuarahia Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward
Rutakangwa (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kumwapisha leo Ikulu
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa
Kipenka na Jaji Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).