Thursday, June 21, 2012

WATANZANIA WATAKIWA KUYAPA MAISHA YAO NAFASI YA KUCHEZA

 Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na maswala ya michezo na Afya Africa, maarufu kama  Right to Play Bw, Peter de Keijzer akizungumza na wajumbe mablimbali wa michezo waliohudhuria warsha ya michezo inayokwenda kwa jina la  Nation Forum on Sport  for Development and peace kuhusiana na namna ya michezo inavyoweza kuleta maendeleo nchiniendapo itapewa kipao mbele na Mtanzania, Bw, Peter alizungumzia baadhi ya faida za kucheza kuwa ni Kuimarisha Afya, ambapo afya ikiimarika tunapata nguvu ya kuleta maendeleo nchini.
 Baadhi ya wajumbe kutoka sehemu mbalimbali waliophudhuria semiana hiyo wakisikiliza kwa makini.

 Waandishi wa habari nao walipata Fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo wanao onekana ni waandishi wa habari wakisikiliza mada kutoka kwa Peter.
Mkurugenzi wa Michezo katika wizara ya habari utamaduni na michezo Bw, LeornadTadeo akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na Semina hiyo ambapo alisema kuwa watoto wanapaswa wapewe nafasi ya kucheza ili tuweze kuwa na taifa la  wachezaji kwakipindi kijacho.