Monday, June 11, 2012

WASANII WAPINGA MFUMO WA DIGITALI WANATAKA ANALOGIA IENDELEE KUPETA


Mhandisi wa mambo ya mitandao katika mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)   Bw, Joel Chacha (katikati) akizungumza na wasanii  katika Jukwaa la sanaa  juu ya mada isemayo,Teknolojia ya Digitali na faida zake katika sekta ya sanaa na wasanii, jukwa hilo lilifanyika leo katika ukumbi wa Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) jijini Dar es Salaam. Katika jukwaa hilo wasanii wengi walionyesha kupinga teknolojia hiyo kwani inaonyesha kuua sanaa yetu kutokana na kuwa, ni watu wachache tu, wenye ndio watakuwa na uwezo wa kununua Vin’gamuzi na mtu wa hali ya chini hatokua na uwezo wa kuwa navyo kulia ni Agnes Kimwaga Afisa mahusiano mkuu wa Basata na kushoto ni  Katibu mtendaji wa Basata Bw, Ghonche Matenego.

Bw, Joel Chacha akiongea na mwandishi wa habari katika Jukwaa hilo