Raisi wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Bw, Gratian Mukoba (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari juu ya maazimio yao katika baraza la Taifa
kuhusu nyongeza ya mishahara na posho ambapo alisema kuwa wanataka matatizo yao
kujadiliwa ikiwemo posho pamoja na
nyongeza ya mishahara kwa asilimia mia moja. Aidha Bw, Mukoba alisema
kuwa,mabali na kupewa posho pamoja na kuongezewa mishahara pia wanaitaka
serikali iwalipe deni lao la kiasi cha sh, Bilioni 13 kwa kukazia hilo Rais huyo alisema kuwa kufikia tarehe sat mwezi wa saba mwaka huu watajua la kuwaambia walimu ikiwa bado hawajapewa jibu la malalamiko yao.
|