Wednesday, June 20, 2012

WANANCHI WA DAR ES SALAAM WATAKIWA KULIMA MPUNGA MABONDENI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Said Meck Sadick akiongea na wajumbe  wa zao jipya la Mpunga leo, kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonyesho hayo, ambapo alisema kuwa wananchi waishio Dar es Salaam wanapaswa kutumia mabonde waliyonayo kulima zao la mpunga badala ya kutegemea Mchele kutoka sokoni tu.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akisikiliza namna zao la mpunga linavyoweza kulimwa bila kutegemea mvua kutoka kwa mkurugenzi wa Tanseed Internation Ltd Bw,Saka Mushauri ambapo alisema kuwa zao hilo linaweza kulimwa mahali popote hata kwenye Magorofa kwa kumwagilia.