Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nation Health Insurance Fund (NHIF) Bw, Eugen Mkongoti akizungumza na vikundi mbalimbali vya kina mama wapatao (400) wanaopatiwa elimu juu ya umuhimu na faida za kuwa mwanaschama katika mfuko wa Bima ya Afya ambapo alisema kuwa watapata fursa ya kupata matibabu bure kwa watu sita katika familia ambao watakuwa ni Mme na Mke pamoja na watu tegemezi wanne kwa mwanachama mmoja atakayekubali kuwa mwanachama wa NHIF mfuko wa Bima ya Afya mafunzo hayo yanaendelea hivi sasa katika ukumbi ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM.
Kaimu mkurugenzi wa Bima ya Afya Bw, Rehani Athmani akikazia umuhimu wa kinamama kujiunga na kuwa wanaachama katika mfuko huo.
Mkurugenzi Idara ya Uwezeshaji Wanawake (WAMA) Bi, Tabu Likoko akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya namna wanawake watakavyofaidika watakapo amua kuwa wanachama wa mfuko wa Bima ya Afya.
Baadhi ya kinamama walioghudhuria katika mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini.