Tuesday, June 5, 2012

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WATOA MAKAKATI WA KUDHIBITI BIASHARA YA MAZAO YA MISITU KINYUME CHA SHERIA

Mtendaji mkuu wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania (kulia) Bw, Juma S Mgoo akizungumza na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa Wizara ya maliasili na Utalii Jijini Dar es Salaam, juu ya Mkakati wa kudhibiti biashara ya mazao ya misitu kinyume cha sheria pamoja na kuboreshaukusanyaji maduhuli, ambapo alisema kuwa,wakala umefanya ukaguzi maalum wa namana biashara ya mazao ya misitu naukusanyaji maduhuli inavyosimamiwa katika maeneo mbalimbaliili kubaini na kujionea hali halisi katika kudhibiti biashara ya mazao ya misitu na kukusanya maduhuli kwa nchi nzima kuanzia tarehe 7/05-21/05/2012 kushoto ni Kaimumkurugenzi wa utunzaji wa rasilimali za misitu Bw, Daudi Mbwambo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbaliwaliohudhuria katika mkutano huo.