Wednesday, June 6, 2012

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA KWA WAATUMIAJI WA INTERNET

Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame Makundi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo hii katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa huduma mpya ya tigo inayokwenda kwa jina la 'TIGO INTERNET MEGA BOKSI' ambapo alisema kuwa wateja watigo wataweza kujipatia vifurushi vipya vya mtandao vinavyo endana na mahitaji yao. Makundi alisema kuwa Mteja wa Tigo ataweza kununua kifurushi cha siku, wiki, au mwezi  pamoja na kufanya uchaguzi unaoendana na  matumizi mbali mbali ya huduma za kimtandao.alielezea namna ya kupata vifurushi hivyo kuwa ni, kwa kupiga *148*01# ambapo wateja watapata fursa ya kuchagua muda wa  viofurushi wanavyovihitaji kulia ni Alice Maro afisa habari wa Tigo.
Alice Maro afisa habari wa Tigo akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari alipoulizwa kuhusiana na huduma hiyo mya.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakifwatilia uzinduzi wa huduma hiyo.
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame Makundi.