Friday, June 1, 2012

WADAU WA SENSA WAANDAA BILIONI 141.5 KWA AJILI YA KUFANIKISHA ZOEZI ZIMA LA SENSA

Mkurugenzi wa Operesheni ya Takwimu  Bi,  Radegunda Maro  (kulia) akiongea na wamiliki mbalimbali wa vyombo vya habari nchini  juu ya namna ya Uelimishaji jamii kwenye Sensa inayotarajia kuanza mapema mwezi ujao  tarehe 26 ambapo alisema kuwa wao kama tume nzima wamejipanga sdawasawa katika uelimishaji wa jamii juu ya swala hilo la sensa. Mkutano huo umefanyika leo katika Hoteli ya PeakCook jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Sensa nchini  Bi, Hajjat Amina  Mrisho (kushoto) akielezea namna walivyojipanga kushirikiana na vyombo vya habari katika mkutano huo ambapo alisema kuwa wametenga kiasi cha Bilioni 141.5 kwa ajili ya kuhakikisha kuwa swala hilo linakamilika ipasavyo. kulia ni Mkurugenzi wa operesheni ya Takwimu Bi,  Radegunda Maro
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Bw, Kiondo Mshana wa kwanza kushoto pamoja na wakurugenzi wengine  wakisikiliza kwa makini mjadala huo.
Baadhi ya wamiliki mbalimbali wa vyombo vya habari waliohudhuria katika mkutano huo
Mwandishi wa habari kutoka wapo Radio Bw, Willison Kibubu akiuliza swali kwenye mkutano huo