Wednesday, June 13, 2012

VODACOM YABORESHA HUDUMA YA DSTV MOBILE.






Dar es Salaam 12 june 2012. Mashabiki wa soka nchini kote sasa wanaweza

kufurahia mechi za Euro 2012, kupitia simu zao za mkononi, Baada ya Dstv Mobile
na Vodacom Kushirikiana kutoa huduma ya kibiashara iliyosubiliwa kwa muda mrefu
kupitia mtandao wake wa  3G.

Huduma hiyo ya kibiashara imekuwa ikitolewa katika kipindi cha majaribio kwa

mwaka mmoja  na sasa itawapa uwezo maelfu ya watanzania kupata huduma hiyo
ambayo imekuwa gumzo kusini mwa jangwa la sahara.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa hii ni nafasi

ya kipekee kwa wateja wa Vodacom kufurahia huduma hiyo.

“Huu ni ushirikiano Mkubwa kati ya Vodacom Tanzania na Dstv Mobile na tumepanga

kuwapatia wateja wetu huduma nzuri, Tunafurahia kuwa katika ushirikiano huu
maana itawawezesha wateja sio tu kupata taarifa bali hata kuburudika bila kujali
mahali walipo”

Ili kupata huduma hii ya Dstv Mobile ukiwa na simu yako inayowezeshwa na mtandao

wa  3G unakwenda katika  m.vodacom.co.tz  na kuanza kupata huduma hiyo moja kwa
moja na hakuna haja ya kunnunua simu nyingine.

“Tunayo furaha kuweza kuwapatia wateja wetu uwezo wa kuangalia vituo mbalimbali

vya Television ikiwemo TBC 1, na huduma hii itakidhi mahitaji ya kila rika, kwa
kuweza kuangalia katuni na kupata taarifa kutoka pande mbalimbali za dunia”
Alisema Felix Sengo, ambaye ni Mkurugenzi wa Dstv Mobile Africa Mashariki.

Vituo vya Televisheni ambavyo wateja wanaweza kuviona kupitia simu zao  ni

pamoja Televisheni ya Taifa ya Tbc 1,  Africa Magic Swahili ambayo inaonesha
filamu za kitanzania, Africa magic kwa filamu za Nigeria, Televisheni  ya
michezo ya Super sport Blits, supersport live events 1 na 2, Chanel O na Trace
Urban kwa muziki kutoka sehemu

mbalimbali duniani, TBN Africa, Cartoon Network na Boomerang kwa ajili ya

burudani kwa watoto.

Mteja anaweza kupata huduma hiyo kwa kuchagua kwa siku shilingi 1500,au  7500

kwa wiki na shilingi 15000 kwa mwezi. Huduma hii inapatikana popote ambapo
mtandao wa 3G wa Vodacom Unapatikana.