VIONGOZI WA JUMUIA YA KIISLAMU
kumb:vjk/01/12
KAMISHNA WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU,
SLP 796
DAR ES SALAAM
YAH: KUTOKUKUBALIANA NA MSIMAMO WA KIKAO CHA
SENSA CHA JUNI 11 MJINI DODOMA
Husika na Kichwa cha habari hapo juu
Kufuatia kikao kilichoitishwa na Idara ya Takwimu ya
Taifa ambacho kiliwahusisha viongozi wa dini za kikiristo na kiislamu
ambacho kilikuwa na Agenda kupokea maoni ya juu mchakato wa sense tunatoa
msimamo ufuatao :
1)Waislamu tumesikitishwa sana na msimamo uliotolewa
na waziri wa Ofisi ya Rais M ahusiano ya jamii na Uratibu wa kutupilia mabali
mapendekezo ya waislamu ya kuingizwa kipengele cha dini na uwakilishi wa
viongozi wa dini katika tume ya Sensa.
2)Tumesikitishwa na jinsi Waziri Steven Wassira
alivyotumia fursa hiyo ya mkutano kuwakejeli viongozi wa kiislamu waliokuwepo
kwenye mkutano kwa kuwaambia kama hamkuelewa somo wenzenu wakristo
wameelewa.
3)Kwakuwa matarajio yetu yalikuwa ni kuingiziwa
kipengele cha dini kwenye dodosa za sense, msimamo huo unaendelea
kuzingatiwa na jamii ya kiislamu kama kanuni muhimu ya ushiriki wao katika
zoezi zima la sensampaka mapendekezo yaliyotajwa hapo juu yazingatiwe.
Tunatanguliza shukrani zetu
Barua hii imetiwa saini na viongozi 31 kutoka jumuia
na taasisi mbalimbali za kiislamu walioshiriki semina hii.